Huduma kwa wahasiriwa wa uhalifu katika Victoria (Services for victims of crime in Victoria - Swahili)

Serikali ya Victoria kupitia Simu ya Msaada ya Wahasiriwa wa Uhalifu inatoa abari za bure, ushauri na msaada bure kwako na familia yako.

Simu ya Msaada kwa Wahasiriwa wa Uhalifu

Inafunguliwa: saa 2 asubuhi – saa 5 usiku (8am-11pm), siku 7 kwa wiki
Piga simu: 1800 819 817
Ujumbe: 0427 767 891
Barua pepe: vsa@justice.vic.gov.au

Piga simu, tuma ujumbe au barua pepe kwa Simu ya Msaada ili:

  • kujua jinsi ya kuripoti uhalifu kwa polisi
  • kupata huduma nyingine ambazo zinaweza kukusaidia
  • kupata habari kuhusu jinsi mfumo wa hakiwa Victoria unafanya kazi
  • kupata msaada ikiwa unahitaji kuwa shahidi mahakamani
  • kupata msaada wa kuomba kwa fidia na msaada wa kipesa – ikiwa unastahiki
  • Tafuta nini unaweza kufanya ili kukuokoa wewe na familia yako.

Ikiwa uko katika hatari sasa hivi, pigia simu polisi kwa Sifuri Tatu (000). Unaweza pia kwenda kituo cha polisi.

Tunawasaidia watu katika hali nyingi tofauti

Kila mwaka, tunasaidia maelfu ya watu wenye umri tofauti, jinsia na asili ambao ni waathiriwa wa uhalifu.

Tunaweza kusaidia hata kama hautaki kuripoti uhalifu huo kwa polisi

Kuna sababu nzuri za kuwaambia polisi kuhusu uhalifu. Watachukua ripoti yako kwa umakini na kujaribu kumtafuta mtu aliyefanya uhalifu. Wanaweza pia kukulinda.

Ikiwa hauko tayari kutoa ripoti au una wasiwasi juu ya kuzungumza na polisi, Simu ya Msaada:

  • itaongea nawe na kuelewa hali yako
  • itatafuta huduma ambazo zinaweza kukusaidia, hata kama hautaki kuripoti uhalifu
  • itakusaidia kuongea na polisi, ukitaka.

Unaweza kutumia mkalimani

Simu ya Msaada itakupa mkalimani wa bure ikiwa unahitaji mmoja. Unaweza pia kuomba mtu mwingine kupiga Simu ya Msaada ili akupatie mkalimani.

Kupata mkalimani:

  1. piga simu kwa Simu ya Msaada kwa 1800 819 817
  2. uwambie jina lako, nambari ya simu na lugha yako
  3. mkalimani atakupiga simu tena.

Wakati mkalimani anapiga simu, inaweza kuonyesha kama 'nambari ya faragha', 'imefungwa' au 'hakuna kitambulisho cha mpigaji' ('private number', 'blocked' or 'no caller ID' ) kwenye simu yako ya mkononi.

Services for victims of crime in Victoria - information in Swahili (Kiswahili)
PDF 135.52 KB
(opens in a new window)

Updated